Mwangi willy.
Eldoret.
07/7/2011
Zamani tahasubi ya kiume ilikuwa ni tatizo kubwa kwa maeneo yote tunako toka na kwa taifa lote kwa ujumla.
Baada ya mashirika mengi ya kijamii kuingilia kati swala hili,watekelezaji wameanza kutumia mtindo mpya kuiendeleza peupe bila kugunduliwa na wale wenye nia ya kuikomboa jamii kutoka kwenye lindi la tamaduni zilizopitwa na wakati. Ambayo pia nia yao nikuwadhulumu wasio na uwezo,wanyonge na wale wasio fahamu kuwa wanadhulumiwa kwa njia yoyote ile.
Tukisema kuwa Wanawake ndio wanao dhulumiwa, tutakuwa tunakosea pakubwa. Tumewasikia wanaume wengi wakijitokeza na malalamishi yao kwenye viombo vya habari,ya jinsi wanavyoteswa na wake zao;kifisikia na pia kisaikolojia.
Lakini je,yule mtoto wetu wa kike na wa kiume anayesoma Chuo kikuu na anadhulumiwa kimapenzi kwa ajili ya hela tutaita vipi?,tahasubi ya kiume au ya wanajamii nzima?
Wenye hela wote waume kwa wake wanahusika katika kuibomoa mila na desturi waliyotuachia mababu zetu, kwa kuwachafua Watoto wetu.Pesa zinatumiwa kama njia ya kupata mapenzi kutoka kwa wanafunzi wasio na Mapato yoyote zaidi ya pesa za mfukoni kutoka kwa wazazi wao na wale wanao waangalia(guardians).
Jamii imetoka kwa ile enzi ya utumiaji sheria na nguvu kupata unachotaka hadi ule wa uwezo wa kifedha na mamlaka.Ikiwa tutawaachia wale wenye uwezo wa mali na mamlaka kuwatumia watoto wetu kama wanavyotaka,basi tutawapoteza wale ambao wangeisaidia taifa letu siku za usoni.
Ni wazi kuwa vijana wengi chuoni na wale wasio na kazi,wamelambishwa maisha ya anasa wasioweza kuidhabiti wenyewe bila kuwatengemea walio tayari kubadilisha pato lao kidogo kwa raha na uzuri wa maumbile ya wanadamu hawa, wanaotamani maisha mazuri bila jasho.
Ikiwa basi tutaangalia dhuluma ya kijinzia,tusisahau kuaangazia chanzo chake-Malezi mabaya na maisha magumu, ambayo nadhani ndio sababu haswa ya kupotea huku kwa maadili mema ya kijamii.
Walio tumiwa vibaya wakiwa wachanga,wanaingia katika maisha ya ndoa wakiwa wamepoteza hamu ya kuifuraikia maisha ile ya ndoa,na Kinachofuata ni talaka au wanandoa kutoaminiana.
Itatulazimu kuwachunga vijana
wetu kutokana na hadhari ya wenye uchu wa mapenzi;wasio dhamini maisha ya baadaye ya vijana hawa,kwa kuwashauri waidhamini maumbile na maisha yao ya usoni.
Yote tunayoyasikia kwenye vyombo vya habari,namna vijana wengi wanavyo tumbukia kwa anasa na vile maafa inavyowapata,inafaa itupe mwelekeo wa jinsi tunavyo weza kuwatunza watoto wetu na kuwaepusha na ukali wa maisha na madhara mengine yatokanayo na kutojiheshimu kama wanadamu.